PHIT Logo

PHIT Kuwasilisha Tafiti tatu, kutoka Mradi wa Mlinde Mama katika Mkutano wa Tanzania Health Summit, 2026

Prime Health Initiative Tanzania (PHIT) itawasilisha  matokeo kutoka Mradi wa Mlinde Mama katika Mkutano wa 13 wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit – THS 2026), utakaofanyika tarehe 5–7 Oktoba 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Mlimani City, Dar es Salaam. Muhtasari wa tafiti tatu kutoka katika mradi huu umechaguliwa kwa ajili ya kuwasilishwa, na hivyo kutoa fursa ya kushirikisha ushahidi uliopatikana nchini pamoja na mafunzo kutokana na utekelezaji wa kazi za PHIT katika kuboresha afya ya mama nchini Tanzania.

Mada zitakazowasilishwa zitaangazia uzoefu katika kuunganisha Huduma ya Pamoja ya Kliniki kwa Wajawazito (Group Antenatal Care – G-ANC) katika mfumo wa kawaida wa huduma za afya, kupanua matumizi ya teknolojia za kidijitali katika huduma za afya ya mama kwa kutumia akili mnemba, na kuimarisha huduma za uzazi zenye heshima kwa mama wajawazito. Kwa pamoja, mada hizi zinaonesha jinsi tafiti zinazoongozwa na wataalamu wa ndani, ubunifu katika utoaji wa huduma, na matumizi ya teknolojia za kidijitali zinavyoweza kuchangia kuimarisha huduma za afya ya mama na kuboresha uzoefu wa wanawake wanapopokea huduma.

• 05 October 2026
• 08:37
• Mlimani City Conference Center, Dar es salaam, Tanzania
Zinazokuja

Prime Health Initiative Tanzania (PHIT) inafuraha kutangaza kuwa tafiti tatu kutoka Mradi wa Mlinde Mama imechaguliwa kwa ajili ya kuwasilishwa katika Mkutano wa 13 wa Tanzania Health Summit – THS 2026, utakaofanyika tarehe 5–7 Oktoba 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Mlimani City, Dar es Salaam, Tanzania.

Mada hizi tatu zitawasilisha ushahidi na mafunzo yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa Mradi wa Mlinde Mama, zikionyesha kazi ya PHIT katika Huduma ya Makundi kwa Wajawazito (Group Antenatal Care – G-ANC), Njia za kidijitali kwa ajili ya ufuatiliaji wa mama wajawazito kwa kutumia akili mnemba (AI), na pia ujumuishaji wa afua katika mfumo wa afya ili kuboresha tija na kuleta huduma za uzazi zenye heshima (respectful maternal care).

Mada za PHIT Zitakazowasilishwa katika mkutano wa THS 2026, mwezi Oktoba, mwaka 2026

1. Kuunganisha Huduma ya Pamoja ya Kliniki kwa Wajawazito katika Mfumo wa Kawaida wa Afya nchini Tanzania
Mada hii itawasilisha mafunzo yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa Huduma ya Pamoja ya Kliniki kwa Wajawazito katika huduma za kawaida za afya, ikijumuisha masuala muhimu ya kiutendaji katika kuunganisha na kudumisha mfumo huu ndani ya mifumo iliyopo ya afya.
2. Kinachohitajika Kupanua Afua za Kidijitali za Afya ya Mama Tanzania: Mafunzo ya Utekelezaji kutoka Mradi wa Mlinde Mama
Kwa kutumia uzoefu wa mradi katika afya ya kidijitali na matumizi ya akili mnemba (machine learning) katika kutambua wajawazito walio katika hatari, mada hii itachambua mambo halisi yanayoathiri utekelezaji na upanuzi wa ubunifu wa kidijitali katika huduma za afya ya mama nchini Tanzania.
3. Sauti kutoka Wodi ya Wazazi: Jinsi Huduma ya Pamoja ya Kliniki kwa Wajawazito Inavyochangia Huduma za Uzazi zenye Heshima katika Mazingira yenye Rasilimali Chache Tanzania
Mada hii itaangazia uzoefu wa wanawake katika kupata huduma za uzazi na kuchunguza jinsi ushiriki katika Huduma ya Pamoja ya Kliniki kwa Wajawazito unavyoweza kuchangia uzoefu bora zaidi wakati wa kujifungua, unaozingatia taarifa sahihi, msaada, na heshima (respecful maternal care).

Kushirikisha Ushahidi kutoka Mradi wa Mlinde Mama

Mada hizi tatu zinaangazia maeneo tofauti lakini yanayokamilishana ya Mradi wa Mlinde Mama na kuonesha wigo mpana wa maarifa na mafunzo yaliyopatikana kupitia utekelezaji wake.

Kwa pamoja, mada hizi zitaangazia:

• Jinsi Huduma ya Pamoja ya Kliniki kwa Wajawazito inavyoweza kuunganishwa katika huduma za kawaida za afya katika mazingira yenye rasilimali chache
• Masuala muhimu ya kiutendaji katika kupanua afua za afya ya mama zinazotumia teknolojia za kidijitali na ujifunzaji wa mashine
• Mchango unaowezekana wa Huduma ya Pamoja ya Kliniki kwa Wajawazito katika kuboresha uzoefu wa wanawake kuhusu huduma za uzazi zenye heshima
• Mafunzo ya kiutendaji katika kuimarisha huduma za afya ya mama na mifumo ya afya nchini Tanzania

Kuhusu Mradi wa Mlinde Mama

Mradi wa Mlinde Mama ulitekelezwa na PHIT katika Mkoa wa Geita, Tanzania, kwa ufadhili wa Gates Foundation. Mradi uliunganisha Huduma ya Pamoja ya Kliniki kwa Wajawazito kwa makundi (G-ANC) na teknolojia za afya za kidijitali pamoja na kutumia akili mnemba (AI) ili kuimarisha utoaji wa huduma za afya ya mama, kuboresha mwendelezo wa huduma wakati wa ujauzito, na kusaidia kutambua mapema wanawake walio katika hatari kubwa ya kupata matatizo ya ujauzito.

Mradi umezalisha ushahidi muhimu kuhusu utekelezaji wa ubunifu katika huduma za afya ya mama ndani ya mifumo ya kawaida ya afya, ikiwa ni pamoja na mafunzo kuhusu utoaji wa huduma, teknolojia za kidijitali, uzoefu wa watoa huduma na wateja, utayari wa mfumo wa afya, na uendelevu wa afua.

Kuchangia Kujifunza na Kuimarisha Mfumo wa Afya Tanzania

PHIT inatarajia kuungana na watafiti, watunga sera, wataalamu wa afya, watekelezaji wa programu, washirika wa maendeleo, na wadau wengine katika mkutano wa THS 2026 ili kushirikisha matokeo haya na kuchangia mijadala kuhusu kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto mchanga nchini Tanzania.

Kuchaguliwa kwa mihtasari mitatu kutoka Mradi wa Mlinde Mama kwa ajili ya kuwasilishwa kwa njia ya mdomo kunatoa fursa muhimu ya kushirikisha ushahidi uliotokana na mazingira halisi ya Tanzania pamoja na uzoefu wa utekelezaji kwa wadau wengi zaidi katika ngazi ya kitaifa na kikanda.

Ungana Nasi katika mkutano wa THS 2026

Tukio: Mkutano wa 13 wa Tanzania Health Summit – THS 2026
Tarehe: 5–7 Oktoba 2026
Mahali: Kituo cha Mikutano cha Mlimani City, Dar es Salaam, Tanzania

Kwa taarifa zaidi kuhusu Tanzania Health Summit, tembelea tovuti rasmi ya THS au fuatilia Tanzania Health Summit kupitia LinkedIn.

#THS2026 #PHIT #MlindeMama #AfyaYaMama #HudumaKwaWajawazito #AfyaKidijitali #HudumaZaUzaziZenyeHeshima #MfumoWaAfya

Maelezo ya Tukio

• Tarehe 05 October 2026
• Muda 08:37
• Linamalizika 07 October 2026, 17:30
• Ukumbi Mlimani City Conference Center, Dar es salaam, Tanzania

Shiriki

Wasiliana nasi ili kuonyesha nia yako ya kushiriki au kuuliza kuhusu tukio hili.

Shiriki: